Apollo International Patient Services Logo
About Us

Kuhusu sisi

Leo, Hospitali za Apollo zimeweza kusaidia zaidi ya wagonjwa milioni 45 kutoka nchi 121. Hospitali hii ambayo ilianza ikiwa na vitanda 150, inatambulika kuwa mwanzilishi wa hospitali binafsi nchini India, ikiwa na hospitali 64 zinazofanya kazi sasa. Hospitali za Apollo zinajulikana si tu taasisi ya tiba lakini imekuwa kiunganishi kikuu na cha muhimu katika kutoa huduma ya afya bara la Asia, ikijihusisha sana pia katika kutoa ushauri wa kitiba, kliniki, famasia, bima na mazoezi ya aina mbalimbali.

Hospitali ya kwanza kabisa ya Apollo ilianzishwa katika mji wa Chennai, mwaka wa 1983 na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Hospitali, Dr. Prathap C Reddy, ikiwa na lengo la kutoa huduma bora za afya nchini India kwa gharama nafuu ambayo kila mtu India anaweza kumudu. Kabla ya hospitali za Apollo kuanzishwa, ni watu wachache tu walikuwa na uwezo wa kupata huduma za afya bora kwa kuwa waliweza kusafiri nje ya nchi. Huduma zinazotolewa na hospitali ya Apollo ni sawa na zile zinazotolewa katika hospitali nyingine bora lakini kwa kiwango cha gharama ambacho kila mtu anamudu, na hivyo kutokeza mapinduzi katika kuleta huduma bora kwa bei nafuu nchini India. Mpaka leo, mfumo wa kutoa huduma kwa gharama nafuu unaendelea kutumika kama msingi wa mbinu ya matibabu katika hospitali yetu.

IKwa kuongezea, kampuni imejengwa katika mifumo ya misingi imara inayokazia fikra ubora, utaalamu, hisia-mwenzi na uvumbuzi. Kampuni ya Apollo ilikuwa ya kwanza kuweka katika kutambuliwa na kuthibitishwa ubora na jumuiya ya kimataifa kama vile kupitia JCI na pia kuweka vituo vya tiba bora za Sayansi ya moyo, mifupa, neva, huduma ya dharura, Kansa na kuhamisha Viungo. Mfumo wa kuchunguza utendaji wa kazi unatusaidia kutoa huduma zilizo bora. Hospitali za Apollo zinajitahidi kuanzisha miradi ya kusaidia jamii kama vile ACE@25 na TASSC, kuonyesha nia yake ya kutoa huduma bora za kitiba kimataifa.

Maono ya Kampuni

Maono ya Apollo kwa awamu inayofuata ya maendeleo ni ‘Kugusa Maisha ya Bilioni’..

Jua zaidi!